Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 15Article 547096

Habari za michezo of Thursday, 15 July 2021

Chanzo: ippmedia.com

Simba Queens kuongeza 'makali ' kuelekea CECAFA

Simba Queens kuongeza 'makali ' kuelekea CECAFA Simba Queens kuongeza 'makali ' kuelekea CECAFA

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mgosi alisema anaamini mabadiliko hayo ya tarehe hayakufanywa kwa makosa na anaamini muda uliopo ataendelea kukiimarisha kikosi chake ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Mgosi alisema ataendelea kuimarisha wachezaji wake kwa kufanya programu mbalimbali na hatimaye kwenda katika mashindano hayo wakiwa imara zaidi.

"Hatutaathirika na kusogezwa mbele kwa michuano hiyo, tumejiandaa vizuri na baada ya mabadiliko hayo ya kuanza kwa mashindano tumewapa mapumziko ya siku nne wachezaji wetu, tutaingia tena kambini Jumapili ili kuendelea na mazoezi," alisema Mgosi.

Aliongeza kikosi chake kitaendelea kuweka kambi hapa jijini na anamshukuru Mungu hana majeruhi kwenye timu hiyo.

"Awali tulikuwa tunafikiria tutoke kwenda mkoa wa karibu kulingana na hali ya hewa ya baridi ya Kenya, baada ya mabadiliko haya tutabaki Dar es Salaam tukiendelea kujifua, tunataka kwenda huko tukiwa imara zaidi kwa ajili ya kuiletea nchi heshima," alisema Mgosi.

Alisema wanaendelea pia kuwafuatilia wapinzani wao kwa kutizama video za mechi mbalimbali walizocheza kabla ya kuelekea kwenye kinyang'anyiro hicho cha kusaka timu nane zitakazokwenda Misri katika fainali hizo za kwanza.

Simba Queens imepangwa Kundi A pamoja na Lady Doves WFC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Uganda na PVP FC ya Burundi wakati Kundi B linaundwa na New Generation Queens ya Zanzibar, Yel Joint Stars (Sudan Kusini) na timu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia huku FAD ya Djibout na Vihiga Queens ya Kenya zikisalia katika Kundi C baada ya Scandinavia ya Rwanda kujiondoa katika mashindano hayo.

Wakati huo huo, Mgosi ameweka wazi timu hiyo haijamsajili straika chipukizi, Violeth Masele (13), ambaye alionekana katika mchezo wa kirafiki waliocheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), ambao ulimalizika kwa Simba Queens kuchapwa mabao 2-1.

Mgosi alisema alimpa mchezaji huyo ambaye ni mwanafunzi kuonyesha uwezo wake lakini akitarajiwa kwenda kuitangaza Simba Queens atakaporejea masomoni Marekani.