Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 29Article 554233

Soccer News of Sunday, 29 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba Queens ni wababe CECAFA

Mshambuliaji wa Simba Queens akishangilia moja ya magoli waliyofunga Mshambuliaji wa Simba Queens akishangilia moja ya magoli waliyofunga

Kikosi cha Simba Queens kimeanza vyema kukata utepe katika michuano michuano ya Wanawake ukanda wa CECAFA Baada ya kuibugiza PVP ya Burundi mabao 4-1.

Simba Queens ambao ni wawakilishi pekee kutoka Tanzania kwenye michuano hiyo inayoshirikisha Mabingwa wa Nchi za CECAFA imeonyesha ubora na mchezo mzuri mpaka kuibuka na ushindi huo.

Wafungaji wa mabao ya Simba Queens ni Danai Bhobho, Mawete Musollo dk ya 32' na penati dakika ya 81 na Aisha Juma 88 huku bao la PVP limefungwa na Nicole Igilima 52'.

Kwa upande wa Kocha wa Simba Queens Hababuu Omar amesema, kwa matokeo ambayo wameyapata ni silaha kuelekea mchezo ujao.

Amewapongeza wachezaji wake kwa namna ambavyo wamepambana kupata matokeo hayo.

"Vijana wangu wamepambana kupata matokeo sasa tunasubiri mchezo unaofuata naimani tutafanya vizuri pia, "amesema.