Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553921

Soccer News of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba SC waja na mapinduzi ya Kidigitali

Simba SC waja na mapinduzi ya Kidigitali Simba SC waja na mapinduzi ya Kidigitali

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, Leo Agosti 26 wametangaza kuja na mapinduzi ya kidigitali katika utoaji wa taarifa za Klabu hiyo kwa kutambulisha "App" ambayo mshabiki wa Simba anaweza kupata taarifa zote zinazoihusu Klabu ya Simba SC.

Akitoa taarifa hiyo Kaimu Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kupitia "App" hiyo Mashabiki watakua na jukwaa kubwa la kupata taarifa kwa kuwa watakua na uwezo wa kujua kila kitu ambacho kinaihusu klabu.

"Labda tu niwaambie, Mshabiki wa Simba atakua na uwezo wa kujua vikosi katika mechi husika masaa mawili kabla, atajua historia za wachezaji lakini tu niwasisitize kutumia "App" hii kwa kuwa kuanzia leo saa mbili usiku watapata kujua tarehe rasmi ya Tamasha la Simba Day".

"Kupitia "App" hii Mshabiki atakua moja kwa moja amechangia mapato kwa klabu yake na hiyo ni kwa watumiaji wote wa Android na IOS" amesema Kamwaga.

Kamwaga ameongozana na mtaalamu wa masuala ya kidigitali katika kuitambulisha "App" hiyo kwa Waandishi wa habari Given Edward ambaye amesema;

"Matumizi ya "App" hii sio magumu na kama mnavyoona kwa yeyote atakaepata changamoto wapo watu wa kusikiliza na kumuelekeza nini cha kufanya, malipo ni shilingi elfu mbili kwa mwezi kwa kuwa Simba imejali kipato cha kila shabiki wake na unaweza kulipia hata mwaka mzima".

Haya ni Maendeleo ambayo Klabu za Kitanzania zinaendelea kuyaonesha kila leo, Cha msingi ni kusubiti kuona kama wataweza kutimiza yale wanayowaahidi wanachama na mashabiki wao.