Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 16Article 551821

Soccer News of Monday, 16 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba SC yarudi kwa wazawa usajili

Usajili mpya wa Simba, Beki Israel Mwenda Usajili mpya wa Simba, Beki Israel Mwenda

Ni kinyumbani nyumbani sasa katika usajili wa Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba SC.

Simba SC leo imemtambulisha beki Israel Mwenda ikiwa ni muendelezo wa kujiimarisha na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara na ile ya Mabingwa Barani Afrika.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye mitandao yake ya kijamii Simba imeandika;

"Beki mwenye uwezo na sifa za kuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC, Israel Mwenda (21) sasa ni rasmi kuwa ni mchezaji wa mabingwa wa nchi Lion face Karibu Mwenda. Wanasimba tunaamini utaitendea haki jezi ya Simba".

Beki huyo ametokea klabu ya Kindondoni Municipal Council (KMC) na haijawekwa wazi amesaini Mkataba wa Miaka mingapi.