Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 14Article 551545

Soccer News of Saturday, 14 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba Sc wana jambo 2021/2022

Nyota Mpya wa simba, Pape Ousmane kutoka Senegal Nyota Mpya wa simba, Pape Ousmane kutoka Senegal

Ni dhahiri wana jambo msimu wa 2021/2022,ndiyo kauli unayoweza nkusema kwa wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club kwa vurugu wanazozifanya katika soko la Usajili.

Simba wana jambo kuanzia ligi kuu, mpaka michuano ya mabingwa barani Afrika na ndio maana wanasajili wachezaji wazuri kila leo.

Silaha nyingine kwenye kikosi cha Simba,imetambulishwa leo ni nyota kutoka nchini Senegal Pape Ousmane Sakho (24).

Haijulikani kama wekundu hao wa Msimbazi ndio wamefunga usajili ama la. Lakini kwa sasa wako kule nchini Morocco ambapo wameweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi.