Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584716

Soccer News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Simba: Tunawafunga Namungo, tunachukua kombe

Simba: Tunawafunga Namungo, tunachukua kombe Simba: Tunawafunga Namungo, tunachukua kombe

UONGOZI wa Klabu ya Simba umejinasibu kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Namungo utakaopigwa leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, ambapo wametamba kucheza fainali ya michuano hiyo na kushinda kombe.

Simba leo Jumatatu itashuka uwanjani kuvaana na Namungo katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo, itakayopigwa majira ya saa 2:15 usiku.

Mshindi wa mchezo huo anatarajiwa kukutana na mshindi wa nusu fainali ya kwanza kati ya Yanga dhidi ya Azam ambao watacheza majira ya saa 10:15 jioni, katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo itakayopigwa siku ya Alhamisi.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Tunaamini katika ubora wa kikosi tulichonacho, tunajua tutakutana na timu ngumu ambayo mara kadhaa imekuwa ikitoa upinzani tunapokutana.

“Lakini licha ya upinzani huo tunaamini kuwa tutashinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Namungo na tutacheza fainali ambayo niwahakikishie Wanasimba kuwa tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo huo.”