Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 23Article 559252

Soccer News of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba, Yanga ndio muda wa kuonyesha ukubwa wenu

Mokocha wa Simba na Yanga Mokocha wa Simba na Yanga

Jumamosi hii klabu za Simba na Yanga zitashuka dimbani kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ikiwa inaashiria kufunguliwa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2021/22.

Mechi hii inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa sana kwa sababu ya historia ya mechi baina ya timu hizi zinapokutana bila ya kujali aina ya mechi wanayocheza, iwe ya mashindano au kirafiki.

Utamu unaongezeka kutokana na timu zote kufanya usajili wa wachezaji wenye viwango vya juu katika dirisha la usajili. Kila timu iliwachukua nyota ambao inaamini inaweza kuwasaidia katika msimu ujao wa ligi.

Nyota hao licha ya kucheza mechi kadhaa huko nyuma hasa zile za Wiki ya Mwananchi na Simba Day, lakini hapa ndipo wanapoanzwa kupimwa na mashabiki kwa kuona ni jambo gani watalifanya mbele ya watani zao.

Kwa wachezaji wote huu ndiyo muda wao wa kuonyesha timu zote hazikukosea kuwasajili kwa kuonyesha kiwango cha juu katika mechi hii lakini pia katika msimu mzima.

Litakuwa jambo la ajabu sana kwa nyota ambao wanatarajiwa kuwa wataonyesha makali kisha wakashindwa kufanya hivyo. Wachezaji wote fahamuni kwamba mashabiki wanahitaji burudani katika mechi hii.