Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 15Article 551617

Soccer News of Sunday, 15 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba ... hii sasa sifa

Usajili Mpya wa Simba SC, Henock Inonga Usajili Mpya wa Simba SC, Henock Inonga

Ndicho unachoweza kusema mara tu baada ya Klabu ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC, Kushangaza mashabiki wake baada ya kufika ile mida yao (saa tisa mpaka saa kumi na moja jioni) kutambulisha kifaa kipya kama ilivyo Desturi yao.

Leo Agosti 15, majira ya saa tisa alasiri wametambulishha kifaa kingine mpaka wanaogopesha wapinzani wao wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Congo DR na beki kisiki, Henock Inonga Baka (26) ni mchezaji halali wa Simba SC mara baada ya kutambulishwa mda mchache uliopita na Wekundu hao wa Msimbazi.

Kwa namna Simba wanavyofanya usajili wao msimu huu, Inaonekana wachezaji wao wote waliosajiliwa Dirisha hili hakuna aliefikisha umri wa miaka 27, Jambo linalotoa taswira kuwa wana Progrmu ya muda mrefu ndani ya kikosi chao.

Tangu kufunguliwa kwa dirisha hili la usajili,Simba inatambulisha wachezaji wapya mida ya saa tisa mpaka saa kumi na moja jioni katika mitandao yao ya kijamii.