Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573229

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Simba inapiga Sh 500/- ya majengo

Simba inapiga Sh 500/- ya majengo Simba inapiga Sh 500/- ya majengo

Mwenyekiti wa Simba upande wa wanachama, Murtaza Mangungu amefichua kuwa kipato kitokanacho na majengo yao kimeongeza kutoka Sh milioni 200 hadi Sh milioni 500 mara baada ya kuboresha majengo hayo yaliyopo Kariakoo.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Mangungu amesema kuwa lengo lao ni kuendelea kujipambanua kwa kujenga ukumbi na ofisi za klabu ili wanachama na mashabiki waweze kutembelea.

Aidha, Mangungu amegusia suala la uboreshaji wa Uwanja wao wa Mo Arena uliopo Bunju Dar es Salaam, ambapo amesema licha ya ukarabati ila wamepanga kuonheza idadi ya viwanja.

"Uendelezaji wa uwanja wa Mo Arena tumepanga kuendeleza kuanzia hosteli, mabwawa ya kuogelea, kituo cha watoto na kuongeza idadi ya viwanja. Lakini pia tunaangalia namna bora ya kuwashirikisha kwenye ujenzi wa ukuta."Mangungu.

"Kama ilivyo malengo ya Simba ni kuhakikisha tunashinda na kutwaa mataji. Nawaomba tuendelee kushirikiana ili tufanikishe jambo hili."ameongeza Mangungu.