Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558784

Soccer News of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba kuanzia ugenini Ligi ya Mabingwa, Ratiba hii hapa

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika, Simba Sports Club, wataanza kutupa karata yao ya kuwania kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa ugenini.

Simba watasafiri mpaka nchini Botswana kuwavaa Jwanang Galaxy katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kati ya Octoba 15-17.

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, klabu ya Yanga wametolewa katika hatua ya awali na Timu ya Rivers United kutokea nchini Nigeria.