Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 26Article 539950

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Simba kuishukia Dodoma Jiji leo

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Simba leo wataikaribisha Dodoma Jiji katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Mkapa, wakati Dodoma Jiji waliiondoa KMC kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza kwa Simba ambayo Jumamosi iliyopita iliondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-3 na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Timu hizo zinakutana huku wenyeji Simba wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutokana na ubora wa kikosi chake ikilinganishwa na cha wapinzani wao Dodoma FC ambacho kimepoteza mechi zote mbili zilizopita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema wapo tayari kwa mchezo huo na wameupa uzito mkubwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi na kuweka hai matumaini yao ya kutetea taji hilo kwa mara ya pili mfululizo. Alisema wachezaji wake Taddeo Lwanga na Joashi Onyango ambao waliumia kwenye mchezo na Kaizer Chiefs wanaendelea vizuri na huenda akawatumia.

Alisema kikosi chake hakitakuwa na mabadiliko makubwa na kile kilichoikabili Kaizer Cheifs, huku akiahidi kutoa nafasi kwa baadhi ya wachezaji akiwemo mshambuliaji Meddie Kagere na beki Kennedy Juma ambaye aliingia kwenye mchezo dhidi ya Kaizer.

Join our Newsletter