Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553888

Habari za michezo of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simba kuweka kambi Marekani

Simba kuweka kambi Marekani Simba kuweka kambi Marekani

MWENYEKITI wa bodi ya wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' kupitia mitandao yake ya kijamii ameweka wazi kuwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao ya kikosi hicho yatafanyika Marekani.

Bilionea huyo aliandika kupitia mitandao yake ya kijamii "Ilikuwa ni furaha kukutana na Jason Levien ambaye ni mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya DC United ambayo ina thamani ya dola za Kimarekani milioni 700," aliandika na kuongeza;

"Nina furaha kutangaza ushirikiano mpya kati ya klabu za DC United na Simba.

"Ifikapo mwaka 2022 klabu ya Simba itasafiri kwenda Marekani kwa ajili ya mazoezi na maandalizi ya msimu mpya na pia itashiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayo andaliwa na klabu ya DC United, ambayo yatahusisha Ligi ya MSL na klabu kutoka Amerika ya Kusini."

Habari hiyo ni njema kwa kikosi cha Simba kwani wakati huu wanaendelea na maandalizi ya msimu ujao wakiwa Morocco na kundi la mwisho kurejea nchi litafika Septemba 4.

Tangu kuingia kwa Mo Dewji katika kikosi cha Simba kwenye miaka mitano ameipeleka timu hiyo Afrika Kusini mara mbili kufanya maandalizi ya msimu, Uturuki, Morocco na msimu ujao wataenda Marekani.