Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 19Article 547462

Habari za michezo of Monday, 19 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Simba mara 4, Bocco kinara

Simba mara 4, Bocco kinara Simba mara 4, Bocco kinara

PAZIA la Ligi Kuu ya Tanzania Bara limehitimishwa rasmi huku Simba ikikabidhiwa taji lao la nne baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Namungo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mabao ya John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu aliyefunga mawili yalitosha kuifanya Sinba kumaliza msimu kwa kishindo.

Simba imemaliza ligi ikiwa na pointi 83 huku nahodha wake John Bocco akiibuka mfungaji bora akiwa ameweka wavuni mabao 16 huku nafasi ya pili akishika Chris Mugalu akiwa na mabao 15 na Prince Dube akishika nafasi ya tatu akiwa na mabao 14.

Mbeya City imeutumia vyema Uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine, baada ya kuichapa Biashara United Mabao 4-0 na kufikisha pointi 42 na kuivusha hadi nafasi ya 10 katika msimamo na kuishusha Ruvu Shooting hadi nafasi ya 11.

Mabao ya Mbeya City katika mchezo huo yalifungwa na Juma Liuzio aliyefunga mabao matatu na Siraji Juma, Katika mchezo mwingine Azam FC, iliibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Azam imemaliza ligi ikiwa na pointi 68 huku Ruvu Shooting ikiporomoka hadi nafasi ya 11 ikiwa na pointi 41.

Kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma, wenyeji Dodoma Jiji, walishindwa kutumia vema Uwanja wao kwa kutoka suluhu na Yanga.

Polisi Tanzania ikiwa nyumbani Ushirika imemaliza msimu kwa suhindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui.

Kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Tanzania Prisons, wamevutwa shati na kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Gwambina, ambao walikuwa wanasaka nafasi ya kusalia Ligi kuu Bara.

KMC wakiwa katika Uwanja wa Uhuru, wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu na kufikisha pointi 48 na kujihakikishia nafasi ya tano huku wakiiteremsha daraja timu hiyo kutoka wilayani Mbeya.

Timu zitakazoshinda kwenye Play Off zitacheza Ligi Kuu zikiungana na Mbeya Kwanza na Geita Gold zilizopanda msimu huu, na 12 zilizobaki kufanya timu 16 kucheza Ligi Kuu.