Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 552022

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba waendelea kuongeza majeshi

Abdulsamad Kassim Ali, usajili mpya wa Simba Abdulsamad Kassim Ali, usajili mpya wa Simba

Kama ilivyo ada, kwa takriban majuma mawili sasa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba, kila ifikapo saa tisa mpaka saa kumi na moja jioni wao hutambulisha nyota mpya waliemsajili kwa ajili ya msimu ujao.

Leo agosti 17, ilipofika saa tisa wamemdondosha kiungo Abdulsamad Kassim Ali kutokea katika klabu ya Kagera Sugar.

Kiungo huyo haijawekwa wazi amesaini kandarasi ya miaka mingapi lakini ni ingizo jipya kwa mabingwa hao mara nne mfululizo wa nchi.

Katika utambulisho wake kiungo Abdulsamad amesema awatoe shaka kwa mashabiki na viongozi kwani lengo la ujio wake ni kuongeza nguvu ili waweze kushinda mataji.