Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 18Article 558187

Habari za michezo of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Simba waomba radhi mashabiki

Simba waomba radhi mashabiki Simba waomba radhi mashabiki

Club ya Simba imewaomba radhi Mashabiki kutokana na usumbufu wanaoupata wakati wa kununua tiketi kwa ajili ya Tamasha la Simba Day.

Simba imesema usumbufu huu unatokana na mfumo wa N Card ambao umeonekana kutokidhi mahitaji na uwezo wa kuhudumia umati mkubwa wa wapenzi wa mpira katika kipindi kifupi.

“Club imejaribu mara kadhaa kuzungumza na Wahusika wa mfumo huo ili kutafuta suluhu lakini kadri muda unavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya, Mashabiki tunaomba muwe watulivu wakati Club ikiendelea kutafuta suluhisho la kudumu”