Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 27Article 553972

Soccer News of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba yaendeleza Sare Morocco

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Peter Banda akiwania mpira na golikipa wa Kiungo mshambuliaji wa Simba, Peter Banda akiwania mpira na golikipa wa

Klabu ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC imeendelea kutoa sare katika mechi zake za kujipima nguvu dhidi klabu za nchini Morocco.

Simba ambayo safari hii wamecheza na klabu ya Ligi daraja la kwanza ya nchini Morocco, Olympique Club De Khourigba na kutoa sare ya goli 1-1.

Ni Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la mpinzani dakika ya 37 kwa goli la nyota mpya wa Club hiyo Winga Pape Sakho.

Khourigba nao hawakua nyuma kwani dakika ya 61, Adama aliwasawazishia na kufanya mchezo huo kuisha kwa sare ya goli 1-1.

Simba wanatarajiwa kutua nchini wikiendi hii na watajiunga na kambi kwa mara ya pili ingawa bado haijafahamika kambi hiyo itakua wapi.