Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 04Article 545191

Soccer News of Sunday, 4 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simba yafungwa tena

Simba yafungwa tena Simba yafungwa tena

SIMBA imeendelea kusota mbele ya Yanga baada ya kutopata ushindi katika mechi nne za Ligi Kuu walizocheza msimu wa 2019/20 na 2020/21.

Simba msimu wa 2019/20 walitoka sare ya 2-2 na kuja kufungwa bao 1-0 na Bernard Morrison mbele ya Hayati John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano.

Msimu huu wameendeleza tena kupata sare ya bao 1-1 mzunguko wa kwanza na leo kufungwa bao 1-0 lililowekwa wavuni na Zawadi Mauya mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba ndiye mwenyeji wa mchezo wa huo, huku wanamsimbazi wakishindwa kuamini walichokiona.

Wakati huo huo Simba leo imeshindwa kutimiza adhima yao ya kutangaza ubingwa Baada ya kukibali kipigo hicho.

Leo kama Simba angeshinda angetangaza ubingwa mara nne mfululizo licha ya kuwa na michezo minne mkononi.