Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 25Article 559570

Soccer News of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba yalamba dili mpya, yapewa basi tatu

Viongozi wa Simba na wa Kampuni ya Africarriers Viongozi wa Simba na wa Kampuni ya Africarriers

Klabu ya Simba SC, imeingia mkataba wa miaka minne kati yake na kampuni ya magari(Africarriers Limited) wenye thamani ya Shilingi milioni 800 na watapewa mabasi matatu kwa ajili ya timu ya vijana, timu ya wanawake na timu ya wakubwa.

Africarriers ni kampuni ambayo inajihusisha na biashara ya kuuza na kukopesha magari nchini.

Ndani ya Mwezi mmoja Simba SC kupitia Mtendaji wake mkuu, Babra Gonzales wameingia mikataba mitatiu yenye manufaa kwa Kampuni tatu tofauti.

Kampuni hizo ni ATCL,Emirate aluminium na Africarriers, na huu wa sasa unakwenda kuzigusa mpaka timu ya Vijana ya Simba na Timu ya Wanawake.