Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 22Article 552904

Soccer News of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba yalazimisha sare Morocco

Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kusawazisha goli Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kusawazisha goli

Wekundu wa Msimbazi na Mabingwa wa TPL msimu uliopita, leo wamepiga show moja ya kibabe pale nchini Morocco baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya AS FAR Rabat ya nchini humo.

Kikosi cha Simba kwa mara ya kwanza kimecheza mechi ya kirafiki dhidi ya AS FAR Rabat ya nchini humo na kumaliza kwa sare ya mabao 2-2.

Simba ilipanga kucheza mechi tatu za majaribio katika kambi yao na tayari ya kwanza imemalizika kwa sare huku winga mpya Pape Ousmane Sakho akifungua kibubu cha mabao kwa Wekundu wa Msimbazi.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Simba kuwa nyuma kwa mabao mawili na baada ya kurudi kipindi cha pili Hassan Dilunga 54' alitupia bao moja na Sakho kumalizia la pili 81'.

Rabat inanolewa na aliyekuwa kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ambaye aliondoka na nafasi yake kuchukua Didier Gomes.