Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 18Article 552133

Soccer News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simba yanukia pesa

Kikosi cha Simba kikiwa Mazoezini, nchini Morocco walikokwenda kuweka Kambi Kikosi cha Simba kikiwa Mazoezini, nchini Morocco walikokwenda kuweka Kambi

Siku chache baada ya klabu ya Simba kuthibitisha kutokuwa na nyota Clatous Chama na Luis Miquissone msimu ujao, uongozi umefunguka sababu za kuwauza nyota hao kwa pesa ndefu.

Mjumbe wa Kamati ya Usajili, Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi wa Simba, Crensentius Magori, amesema kuondoka kwa Miquissone ni mipango ambayo ilikuwepo kutokana na ofa lakini suala la Chama kwao ni sapraizi.

“Miquissone kwanza kiwango cha fedha anachokwenda kulipwa ni karibu mara nane ya alichokuwa analipwa hapa, hivyo ilikuwa ni ngumu kwao kumzuia asiondoke, anaenda timu kubwa na analipwa vizuri, tulijiandaa kabisa kumuacha,” amesema na kuongeza kuwa:

“Kwa ishu ya Chama ni kitu ambacho kimekuja tukiwa hatuna mpango kabisa, kibaya zaidi msukumo umetoka kwa mchezaji mwenyewe ambaye alituambia kuwa kwenye maisha yake ya soka hajawahi kucheza misimu mitatu kwenye timu moja, hivyo anaomba kuondoka,” amesema.

Magori amesema Chama alianza kwa kupambana na kocha ambaye pia alikuwa haelewi na hakubaliani na hilo, lakini akabainisha kuwa vita ya pili ilikuwa ni dhidi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji “Mo Dewji’ ambaye alikataa, lakini wao kama washauri walikaa chini na kushauri aruhusiwe kuondoka.

“Ndugu yangu tukimzuia huyu mchezaji ndio kwanza kasaini miaka miwili kwa gharama kubwa na bado anakoenda ni mara tatu ya huku, tukimuacha atakuwa na kinyongo na kushindwa kufanya vizuri. Tayari ameshatupa kila kitu kwa miaka mitatu Simba, hivyo acha tumuache aende,” amesema.

“Hauwezi kuamini Chama amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ambao angeanza kuutumikia msimu ujao na makataba huo hakuna mchezaji yeyote Tanzania ambaye anaweza kulipwa lakini bado wenzetu wameweka mara tatu ya huu, hatukuwa na namna nyingine zaidi ya kumuachia aende,” amesema.

Magori amesema Chama alikuwa mchezaji mkubwa na alivyokuja Simba ameongezeka kukua hivyo kuondoka kwake sio kitu kidogo na ndio maana mijadala imekuwa mingi.

Alisema skauti ya kupata mchezaji kama Chama ilikuwa ngumu sana kwao kupata mtu kama yeye ili aweze kuingia moja kwa moja kwenye timu lakini wamefanya kazi ngumu kupata warithi wa wachezaji hao.