Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 551965

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba yashikwa pabaya sakata la Mhilu

Mchezaji anaegombewa na Simba na Kagera, Yusuph Mhilu Mchezaji anaegombewa na Simba na Kagera, Yusuph Mhilu

Siku chache baada ya Mabingwa wa nchi,Simba SC kumtambulisha nyota mpya kutoka klabu ya Kagera Sugar,Yusuph Mhilu kuna taarifa zinazodai kuwa klabu hiyo haikufuata utaratibu.

Mhilu ambae alitambulishwa na Simba Agosti 4,Mwaka huu inadaiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ya Kagera.

Inadaiwa kuwa mazungumzo ya awali, Simba waliwasilisha Ofa ya Mil 35 lakini Kagera wakaipiga chini wakitaka Mil 50 ili wamtoe Mhilu

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Simba wakamtambulisha Yusuf Mhilu, kitendo kilichowakwaza viongozi wa Kagera wakihisi 'kudharauliwa'

Baadae mmoja wa viongozi wa Simba aliwaomba radhi Kagera kuwa utambulisho ule ulifanywa kimakosa na mtu mmoja wa Idara ya Habari, hivyo wakawaomba wasikanushe chochote huku mazungumzo yakiendelea

Lakini Kagera wakashtuka baada ya kuitwa TFF kuwa wamefunguliwa mashitaka na Mhilu akitaka kuvunja mkataba

Na baada ya kesi kusikilizwa na Kagera kuonekana wana haki na Mhilu anatakiwa kufata Taratibu vizuri za Klabu ili kuvunja mkataba, Uongozi wa Kagera sasa Umepanga kuishitaki Simba kwa kumtambulisha mchezaji wao na kuhitaji kiasi cha TSH MIL 200 ili wamruhusu.

Katika kutafuta ukweli wa sakata hilo, Uongozi wa kagera Sugar kupitia Katibu Mkuu wake Masoud Ally wametanabaisha kama Simba hawatatimiza ofa waliyoiweka mezani juu ya kumuuza mchezaji wao Yusuph Mhilu, mchezaji huyo hatoruhusiwa kuichezea klabu ya Simba ambayo ilimtangaza hivi karibuni kuwa ni mchezaji wao.

Akisisitiza Katibu huyo amesema kuwa utambulisho wa kumsajili Mhilu ndani ya Simba ulifanyika kimakosa kutokana na pande hizo mbili kutokuwa na maelewano kutokana na Mhilu kuwa na mkataba wa Mwaka mmoja na Kagera ambao simba walikuwa bado hawajaununua.

“Simba walimtambulisha Mhilu kimakosa, uzuri waligundua hilo wakatuomba radhi, Mhilu bado anamkataba wa msimu mzima na Kagera Sugar, hiki kinachofanyika ni biashara na mtu anapoleta ofa yake na sisi tunakuwa na ofa yetu.

“Ofa tuliyowapa Simba juu ya kununua mkataba wa Mhilu bado haijatimizwa na Kuna muda uliowekwa wakufanya makubaliano hayo Kama huo muda utafika na Simba wakawa bado hawajatimiza hilo basi Mhilu atabaki kuwa mali ya Kagera na hata ruhusiwa kuichezea simba,” amesema Masoud.