Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553879

Soccer News of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba yawatoa nyota wake kwa mkopo

Kiungo wa Simba, Said Hamisi Ndemla Kiungo wa Simba, Said Hamisi Ndemla

Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba, wamethibitisha kuwatoa kwa mkopo kwenda timu tofauti nyota wake David kameta 'Duchu',Ibrahimu Ame na Hamis Ndemla.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo Duchu ameelekea Biashara United Mara, Ibrahimu Ame na Ndemla wamejiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Mabeki hao walijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita huku Ame akitokea Coastal Union ya Tanga kama mlinzi wa kati wakati Duchu akitokea Lipuli ya Iringa kama mlinzi wa pembeni.

Kwa upande wa Ndemla yeye ni wa muda mrefu ndani ya Simba na mara kwa mara wadau wa soka nchini wamekua wakimpigia kelele atafute sehemu atakayopata nafasi ya kucheza.