Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 09Article 562225

Michezo Mingine of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simbu akwaa kisiki tena riadha taifa

Simbu akwaa kisiki tena riadha taifa Simbu akwaa kisiki tena riadha taifa

Ndoto ya nyota wa mbio ndefu za barabarani (marathoni), Alphonce Simbu kutwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya taifa ya riadha imeyeyuka rasmi baada ya kuikosa kwa mara nyingine katika fainali ya mita 5000.

Simbu ambaye jana aliambulia medali ya shaba kwenye fainali ya mita 10000, leo katika fainali ya mita 5000 ameambulia medali kama hiyo akitumia dakika 14:38:88.

Fabian Nelson wa Arusha ndiye amekuwa kinara kwenye mbio hiyo akitumia dakika 14:14:24 na Faraja Damas Lazaro akimaliza wa pili akitumia dakika 14:26:24.

Lazaro ndiye alitwaa medali ya dhahabu kwenye fainali ya mita 10,000.

Baada ya mbio hiyo, Simbu aliyewahi kuwa mshindi wa medali ya shaba ya dunia alisema amechuana na wakimbiaji wenye mbio yao.