Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 25Article 573934

Soccer News of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Siri yavuja Pochettino kuwachomolea Mabosi wa United

Mauricio Pochettino Mauricio Pochettino

Taarifa za kukataliwa kwa klabu ya Manchester United na kocha wa timu ya PSG zimevuja, ni kuwa klabu ya PSG imeshindwa kumshawishi Zinedine Zidane kuweza kuchukua mikoba ya Pochettino iwapo anaondoka.

Pochettino awali alikuwa anavutiwa kuhamia kwenye klabu ya Manchester United katikati ya msimu endapo klabu ya PSG ingemruhusu kuondoka, lakini haionekani kama inaweza kutokea kwa sasa.

PSG imekataa kumwachia na kuondoa uwezekano kwa klabu ya Man United kumpata kwa sasa kocha huyo raia wa Argentina na kumuhitaji aendelee na majukumu yake mpaka mwisho wa msimu.

Zidane kwa sasa hana kibarua baada ya kuachana na Real Madrid lakini anasemekana anasubiri kwenda kuinoa timu ya Taifa ya Ufaransa.

Kwa sasa klabu ya Manchester United wanaangaika kuweza kumpata kocha wa muda baada ya kumfungashia virago aliyekuwa kocha watimu hiyo Ole Gunnar Solskajaer ambae nafasi yake kwa sasa anasimama mchezaji mwingine wa zamani wa Klabu hiyo Michael Carrick.