Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 08Article 584194

Soccer News of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Son Heung-min kuikosa Michezo yote January

Son Heung-min Son Heung-min

Mchezaji wa klabu ya Tottenham Son Heung-min anaweza kuikosa michezo yote ya mwezi January kutokana na majeruhi ya mguu kwenye mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Chelsea.

Mshambuliaji huyo alifanya vipimo ilikuweza kuangalia tatizo la misuli baada ya kijisikia maumivu kidogo kwenye mchezo wa kwanzawa kombe la Carabao Cup nusu fainali Jumatano dhidi ya Chelsea ambapo Tottenham walipoteza kwa 2-0.

Majeruhi hayo yatamuweka nje kwenye nchezo wa marudiano tena na Chelsea wiki ijayo na pia ataukosa mchezo wa derby ya kaskazini mwa London dhidi ya Arsenal.

Conte wakati akitoa taarifa kuhusu Son alisema, “anaweza kukaa bila ya kufanya mazoezi kwa kipindi cha kati ya 24 January.”

Son Heung-min ndie mfungaji anayeongoza kwenye klabu ya Tottenham msimu huu akiwa na goli nane, alianza kwenye mchezo dhidi ya Chelsea kwenye kombe na alifanikiwa kucheza kwa dakika 79 kabla ya kutolewa.

Ikiwa Son Heung-min hatafanikiwa kurudi uwanjani mpaka mapumziko ya kimataifa kuisha basi atakosa michezo ya ligi kuu ya uingereza dhidi ya Arsenal, Leicester City na Chelsea.