Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552583

Habari za michezo of Friday, 20 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Sports Countdown, Dullah na Kiduku kutwangana leo

Sports Countdown, Dullah na Kiduku kutwangana leo Sports Countdown, Dullah na Kiduku kutwangana leo

Stori kali sita (6) leo kwenye Sports Countdown ya Supa Breakfast ya Eastafrika Radio kuaniza Saa 1:15 asubuhi. Na kila namba unahusiana na stori, na stori kubwa leo ni pamoja na Dullah Mbabe na Twaa Kiduku kunyukana leo, lakini pia Serikali yaweka mpango wa kujenga miundombinu ya michezo.

6. Ni nafasi anayoshikilia Bingwa mtetezi wa michuano ya tennisi ya US Open, Dominic Thiem kwenye viwango vya ubora upande wa wanaume, raia huyoo wa Australia atakosekana kwenye michuano hiyo inayotarajia kufanyika Agosti 30 mwaka huu nchini Marekani kutokana na nyota huyo kujitonesha mkono wake siku ya jana alipojaribu kufanya mazoezi mepesi.

Thiem ameandika kupitia ukurasa wake wa Twetter kuwa hataweza kutetea ubingwa wa michuano ya wazi ya Marekani US Open kutokana na maumivu hayo na amefikia uamuzi huo baada ya ushauri aliopewa na jopo la madaktari wake na kuthibitisha nyota huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwaka mzima.

Mara ya mwisho Thiem kujitupa dimbani ilikuwa ni mwezi Juni mwaka huu kwenye michezo ya Mallorca Open nchini Hispania ambapo alipata maumivu hayo ya mkono.

5. Ni sawa na asilimia ya pesa itayokatwa na Serikali kutoka kwenye pesa zinazotokana na michezo ya kabashiri michezoni hapani nchini, ambapo pesa hizo zitaingia kwenye mfuko wa maendeleo ya michezo na kutumika kutengeneza miundo mbinu ya michezo nchini ili kuhakikisha kama taifa tunakuwa na viwanja vingi vyenye ubora.

Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amethibitisha serikali kuwa kwenye mchakato wa kujenga na kufanya marekebisho ya miundombinu ya michezo nchini na akithibitisha kuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia asilimia 5 ya mapato yanayopatikana kutoka kwenye pesa za michezo ya kubashiri ziingie kwenye mfuko wa michezo, Msigwa amesema lengo nikuhakikisha nchi nzima inakuwa na viwanja vizuri na sio mikoa michache pekee kama ilivyo sasa kwa mikoa ya Dar es salaam na Mwanza.

4. Ni idadi ya wachezaji wa klabu ya Arsenal ambao walikutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona na kusababisha kuukosa mchezo wa ufunguzi wa ligi Kuu England EPL Ijumaa iliyopita dhidi ya Brentford. Wachezaji hao ni nahodha Pierre emerick Aubameyang, Alexander Lacazette Willian na Golikipa wa akiba Alex Runarsson.

Arsenal haikuweka wazi sababu ya Wachezaji hao kuukosa mchezo dhidi ya Brentford ambao walifungwa kwa mabao 2-0, Kabla ya kubainika kuwa wachezaji hao walikutwa na uviko 19. Na inaripotiwa baada ya vipimo kufanyika tena Willian na Aubameyang hawajakutwa na maambukizi hivyo huenda wakawa sehemu ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya mahasimu wao kutoka jiji la London Chelsea mchezo utakao chezwa siku ya jumapili.

3. Ni idadi sawa ya wachezaji na makocha waliorodheshwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA kwenye kinyanganyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora na kocha bora wa mwaka 2021.

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora ni Kevin de Bruyne wa Mancheater City na timu ya taifa ya Ubeligiji, Ngolo Kante wa Chelsea na Timu ya taifa ya Ufaransa na Jorginho nae wa Chelsea akikipiga katika kikosi cha mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Italia wachezaji wote hawa wanacheza katika idara ya kiungo.

Kwa upande wa makocha wanao wania tuzo ni Pep Guardiola kocha wa Mancheater City raia wa Hispania na alikiongoza kikosi chake kutwaa ubingwa wa Ligi kuu England, kocha mwingine ni mjerumani Thomas Tuchel ambaye ni kocha wa Chelsea na alitwaa ubingwa wa vilabu barani ulaya mwaka huu, na kocha wa mabingwa wa Ulaya timu ya taifa ya Italia Roberto Mancini nae yupo kwenye kinyanganyiro hicho. Washindi wa tuzo hizi watatangazwa August 26, 2021.

2. Ni sawa na idadi ya mapambano ambayo watakuwa wamepigana mabondia Dulla Mbabe na Twaha kiduku ambao leo usiku ijumaa Agosti 20 Mabondia Twaha Kiduku na Abdallah Pazi maarufu ‘Dullah Mbabe' watashuka uringo kupambana katika pambano la uzito wa kati ‘’Super Middle weight’’, pambalo la round 12, litakalo fanyika katika ukumbi wa Ubongo Plaza kuanzia majira ya saa 6 usiku.

Mabondia wote wamefanikiwa kupima uzito na afya zao jana mchana kuelekea kwenye pambano hili ambapo mshindi atazawadiwa gari aina ya Toyota Crown Athlete. Hili ni pambano la Pili mabondia hawa wanapigana pambano la kwanza Twaha Kidugu alimtwanga Dullah Mbabe.

Akizungumza na waandishi wa habari promota wa pambano hili kapteni Selemani Semunyu amesema maandalizi yote yameshakamilika huku akiwatoa wasiwasi mashabiki wa ngumi kuwa hali ya usalama itakuwa nzuri kwahiyo wajitokeze kwa wingi kuja kuaangalia ni nani atakae ondoka na gari hilo.

1. Ni mwaka uliosalia kwenye mkataba wa Kylian Mbappe na klabu yake ya PSG na inaripotiwa kuwa mshambuliaji huyo ameuambia uongozi wa PSG kuwa hata saini mkataba mpya na klabu hiyo na anataka kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania, ripoti zinadai kuwa Mbappe alifanya kikao na Rais wa klabu Nasser Al-Khelaifi.

Real Madrid hawajapeleka ofa yoyote kwa PSG ya kumsajili Mbappe ambaye ni mshindi wa kombe la Dunia na timu ya taifa ya Ufaransa 2018 na inaaminika kama PSG watakuwa tayari kumuuza basi Madrid watapeleka ofa yao ingawa mabingwa hao wa Kihistoria wa ulaya wanataka wamsajili katika dirisha la usajili lijalo pindi atakapo kuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika June 30 2022.

Mbappe mwenye umri wa miaka 22 ameshaichezea PSG michezo 173 na amefunga mabao 133 kwenye mashindano yote tangu alipojiunga na matajiri hao wa jiji la Paris msimu wa 2017-18 akitokea AS Monaco.