Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 19Article 552367

Soccer News of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Sports Countdown, Spurs yagoma kumuuza Kane

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane

Stori kali sita (6) ambazo zinatokana na namba 1 mpaka 6 ambapo kila namba inahusiana na stori husika kwenye Supa Breakfast ya Easta frica radio kuanzia Saa 1:15 Asubuhi.

Stori kubwa leo Spurs yagoma kumuuza Harry Kane na Yanga kumsajili mchezaji mmoja.

6. Ni sawa na idadi ya miaka iliyo kwenye mkataba wa mchezaji nyota wa Philadelphia 76ers, Joel Embiid ambaye ameongeza kandarasi ya miaka 4 kwenye mkataba wake, na mkataba wake wa awali ulikuwa umesalia miaka miwili ambao ungemalizika mwaka 2023 lakini sasa ataendelea kubaki na wakali hao wa ligi ya kikapu nchini Marekani hadi mwaka 2027.

Baada ya kusaini mkataba mpya, Embiid ambaye alishika nafasi ya pili kwenye kuwania tuzo ya mchezaji bora wa NBA nyuma ya Nicola Jokic wa Denver Nuggets, amesema hakuna sehemu nzuri ya kuwepo zaidi ya kuwa Philadelphia na sasa yupo tayari kuwania ubingwa wa NBA msimu ujao.

Mkataba wa Embiid una tahamani ya dola za Kimarekani milioni 196 sawa na bilioni 454 na zaidi ya milioni 500 za kitanzania na kumfanya awe mchezaji wanne mwenye mkataba mnono kwenye NBA kwa sasa huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Stephen Curry wa Golden State Warriors mwenye mkataba wa thamani ya milioni 215 dola za kimarekani sawa na zaidi ya bilioni 498 za kitanzania.

5. Ni namba ya Jezi aliyoivaa kiungo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Italia Manuel Locatelli kwenye michuano ya Euro 2020, na kiwango chake bora kwenye michuano hiyo kilimfanya awaniwe na vilabu kadhaa barani ulaya, lakini klabu ya Juventus ndio imefanikiwa kuinasa huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa kumsajili kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili (2) akitokea katika klabu ya Sassuolo lakini mkataba huo ukiwa na kipengele cha Juventus kumnunu mchezo huyo kwa ada ya uahamisho ya Euro milion 25 pindi mkataba huo wa mkopo utakapo malizika pesa hiyo ni zaidi ya bilion 67 na milioni 901 za kitanzania.

Locatelli sifa yake kubwa ni uwezo wa kukimbia eneo kubwa la uwanja na kuanzisha mashambulizi, na akiwa na umri wa miaka 23 ameshacheza jumla ya michezo 144 kwenye Ligi kuu nchini Italia Serie A, na kiungo huyu alikuwa sehemu ya wachezaji ambao kocha wa Juventus Maximiliano Allegri aliuomba uongozi wa klabu hiyo kumsajili sambamba na kiungo wa FC Barcelona Miralem Pjanic.

4. Ni idadi ya mbio za magari za F1 maarufu kama langa langa zilizohairishwa mwaka huu kutokana na janga la virusi vya Corona, idadi hiyo imefika baada ya Serikali ya Japan kuzifuta mbio za Japanese Grand prix kutokana na idadi ya maambukizi ya Uviko 19 kuongezeka nchini humo. Uongozi wa F1 umeweka wazi kuwa utafanyia kazi kalenda ya mbio hizo utajaribu kuweka mambo sawa na watatoa tamko wiki chahche zijazo.

Japanese Grand prix ilipangwa kufanyika kati ya Oktoba 8 hadi 10, na zilipaswa kuwa mbio za 17 kati ya 23 na hii inakuwa ni kwa mwaka wa pili mfululizo mbio hizi zinashindwa kufanyika Japan kutokana na Corona, mbio nyingi ambazo hazikufanyika katika kalenda ya F1 mwaka huu ambazo zilihairishwa ni zile za Australia, China, Canada na Singapore na mbio zinazofata ni Belgium GP zitakazofanyika Agosti 27 mpaka 29 na kalenda ya Langa Langa mwaka 2021 itafungwa kwa mbizo za Abu Dhabi GP kati ya December 10 na 12.

Na katika msimamo wa Madereva Lewis Hamilton wa Mercedes Benz ndio kinara akiwa na alama 195 na nafasi ya pili yupo Max Verstappen wa Red bull mwenye alama 187.

3. Ni miaka iliyosalia kwenye mkataba wa Harry Kane na klabu ya Tottenham Hotspur, na kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini England zinaripoti kuwa Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy hatosikiliza ofa ya timu yoyote inayotaka kumnunua mshambuliaji huyo wakimataifa wa England, klabu ya Manchester City ilishapeleka ofa ya pauni milion100 zaidi ya bilioni 318 kwa pesa za Tanzania kwa ajili ya kumsajili Kane lakini ofa hiyo ilikataliwa na sasa wamejipanga kupeleka ofa ya mwisho ya kumsajili Kane.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alimaliza akiwa kinara wa ufungwa wa EPL Msimu uliopita akiwa na mabao 23 aliweka wazi kuwa alikubaliana na uongozi wa timu hiyo kuwa kama timu hiyo haitashinda kombe lolote na haita maliza katika nafasi nne za Juu kwenye msimamo wa EPL msimu uliopita wa 2020-21 basi ataondoka na Spurs msimu uliopita ilimaliza nje ya nafasi 4 za juu na haikushinda kikombe chochote na sasa mchezaji huyo anataka kuondoka klabu hapo na timu pekee iliyoonyesha nia ya kumsajili ni Manchester City.

Kane hajasafiri na Kikosi cha Tottenham kilichofasiri kuelekea nchini Ureno kwa ajili ya mchezo wa mtoano wa kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundu ya michuano ya Uefa uropa League dhidi ya Pacos De Ferreira ya ureno mchezo utakao chezwa leo usiku majira ya Saa 3 na nusu.  

2. Ni miaka aliyosaini kocha Herelimana Haruna kuwa kocha mkuu wa klabu ya Mbeya Kwanza ya jijini mbeya. Kocha huyo raia wa Burundi ambaye amewahi kuzifundisha timu za VPL Lipuli ya FC ambayo kwa sasa umeshuka daraja lakini pia alikiongoza kikosi cha KMC kwa muda amesaini mkataba huo wa miaka miwili hapo jana na kutambulishwa rasmi na klabu hiyo kuwa kocha mkuu atakayekiongoza kikosi hicho kwenye mikikimikiki ya Ligi kuu Tanzania bara ambapo timu hiyo itakauwa ikicheza ligi kuu kwa mara ya kwanza.

Mbeya Kwanza ilianzishwa mwaka 2012 ikiitwa Coca Cola Kwanza kama timu ya wafanyakazi wa Coca Cola, lakini mwaka 2014 ilibadilishwa na kuitwa Mbeya Warriors ikiwa inashiriki Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL). Hata hivyo mwaka 2015 ikiwa Ligi Daraja la Pili (SDL) ikabadilishwa na kuwa Mbeya Kwanza ambapo jina hilo limeendelea hadi sàsa. Walikata tiketi ya kupanda ligi kuu baada ya kumaliza wakiwa vinara wa kundi A, na waliongoza kundi kwa tofauti ya alama 9.

1. Ni idadi ya mchezaji aliyesalia kutambulishwa kwenye kikosi timu ya Wananchi Young Africans katika dirisha hili la usajili ambalo bado lipo wazi mpaka mwishoni mwa mwezi Agosti.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hersi Saidi amesema bado usajili wa mchezaji mmoja ili kukamilisha zoezi la usajili lakini hawezi kuweka wazi sasa ni mchezaji gani, Kikosi cha Yanga kipo nchini Morocco kikiwa na idadi ya wachezaji 27, kimekita kambi huko ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa mashindano pre-season kuelekea msimu wa 2021-22 na mchezaji pekee ambayo bado hajajiunga mazoezini ni KhalidAucho.

jumla ya wachezaji 10 wapya wametambulishwa rasmi katika kikosi hicho ambao ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yusuph Athuman, Djuma Shaaban, David Bryson, Dickson Ambundo, Erick Johora, Jesus Moloko Khalid Aucho na Djigui Diarra.