Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 05Article 541126

Habari za michezo of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Matola: Simba hakuna kulala

Matola: Simba hakuna kulala Matola: Simba hakuna kulala

KOCHA msaidizi wa timu ya Simba SC, Seleman Matola amesema nia yao ni kupambana na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Matola alisema hayo juzi baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wao wa ligi hiyo dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

‘’Bado tunahitaji pointi sita au tisa na tunapoelekea ni kuzuri, nia yetu kwa sasa ni kutetea ubingwa. Tuna nafasi kubwa sana ya kutetea ubingwa, “alisema Matola.

Alisema mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting ulikuwa mzuri sana na timu yake iliweza kutawala mchezo huo.

‘’Mchezo ulikuwa mzuri sana tuliweza kutawala na kutumia nafasi zetu zote tulizopata. Tulikuwa tunahitaji ushindi kwa hali yoyote ile,’’ alisema Matola.

Kocha huyo wa zamani wa Lipuli FC na Geita Gold Mine alipongeza mchezo safi kutoka kwa mabeki wake, Kenedy Juma na Erasto Nyoni.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting Charles Mkwasa alisema timu yake ilijipanga kushinda, lakini wachezaji wake walifanya makosa.

‘’Tulijipanga kufanya vizuri, lakini tulifanya makosa kipindi cha kwanza wenzetu wakatuadhibu,’’ alisema Mkwasa.

Alisema kipindi cha pili, timu yake ilijaribu kurudi mchezo, lakini kadi nyekundi mbili ziliirudisha nyuma.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba SC ipo kileleni ikiwa na alama 67 baada ya michezo 27 iliyocheza mpaka sasa baada ya kushinda mara 21,sare nne na imepoteza michezo miwili dhidi ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons.

Bingwa huyo mtetezi amefunga mabao 64 na kufungwa 11. Ruvu Shooting katika msimamo ipo kwenye nafasi ya 10 ikiwa na alama 37 baada ya michezo 30. Timu hiyo imefunga mabao 32 na kufungwa mabao 29.

Ruvu Shooting imeshinda mechi 10, sare saba na imepoteza mara 13.

Habari

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni