Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 08Article 561940

Soccer News of Friday, 8 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Stars kusafiri leo kuwafata Benin, watalipa kisasi?

Kikosi cha Taifa Stars Kikosi cha Taifa Stars

Timu ya Taifa “Taifa Stars” inatarajia kuondoka leo saa 6 mchana kuelekea Benin kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022,utakaochezwa Oktoba 10, 2021 Benin.

Taifa Stars itaondoka na Ndege ya Air Tanzania, huku ikiwa na kumbu kumbu ya kupoteza mchezo wa nyumbani kwa goli 1-0.

Katika mchezo huo wa Kundi J, Benin inaongoza kundi hilo ikiwa imejikusanyia alama 7, DR Congo nafasi ya pili wakiwa na alama 5, Stars nafasi ya 3 alama na Madagascar ikiburuza mkia huku kila timu ikiwa imeshacheza michezo mitatu.