Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 14Article 542611

Habari za michezo of Monday, 14 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Stars yaitoa nishai Malawi

Stars yaitoa nishai Malawi Stars yaitoa nishai Malawi

TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars, imefanya vizuri kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Malawi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezwa jana uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, mashujaa wa Stars walikuwa Nahodha John Bocco aliyefunga bao la kwanza dakika ya 68 na Patrick Mwenda aliyefunga la pili dakika ya 75.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mechi hiyo zilikuwa ngumu kwani wapinzani wa Stars walionekana kujipanga vizuri na kutawala mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza vizuri kwa Stars, ambapo wachezaji wake walibadilika na dakika ya 68 Bocco ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akifanya vizuri akavunja ngome ya Malawi na kuandika bao hilo.

Kinda wa Mbeya City, Kibu Dennis ndiye aliyemtenezea Bocco bao hilo. Mshambuliaji huyo alitokea benchi jana.

Kibu alimpasia Bocco pasi murua na bila ajizi mchezaji huyo mkongwe akapachika bao nyavuni.

Kibu pia alisababisha bao la pili ambapo aliangushwa nje kidogo la eneo la hatari na Mwenda akafunga bao la pili kwa adhabu akiapiga mpira uliokwenda moja kwa moja golini.

Kikosi cha Stars : Aishi Manula, Shomari Kapombe/ Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni/ Kennedy Juma, Dickson Job, Mudathir Yahya/ Mzamiru Yassin, Feisal Salum, Salum Abubakar/ Abdallah Seleman, John Bocco, Yussufu Muhilu, Ayoub Lyanga, John Bocco.