Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 551992

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Straika Simba akimbilia KMC

Mshambuliaji alie mbioni kuihama Simba, Miraji Athumani Mshambuliaji alie mbioni kuihama Simba, Miraji Athumani

Klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) inasemekana ipo mbioni kukamilisha usajili wa Mahambuliaji wa Klabu ya Simba SC,Miraji Athumani

Taarifa hiyo inasema kuwa KMC wanamtaka mchezaji huyo ili kwenda kuongeza kasi kwenye safu yao ya ushambuliaji kwa sababu kuna wachezaji wao wengi watarejea kwenye timu zao baada ya mkopo kumalizika.

Mmoja wa wadau wa soka aliye karibu na KMC amesema: “Sheva anasubiri kutambulishwa wakati wowote na KMC kwa sababu mazungumzo baina yao yanakwenda vizuri kabisa.”

Alipotafutwa Msemaji wa KMC, Christina Mwagala alisema: “Sisi hatusajili mitandaoni, wachezaji ambao tutamalizana nao tutawatangaza pale kila kitu kikienda sawa.”

Sheva alikosa nafasi ya kucheza msimu uliopita, baada ya mwaka wake wa kwanza Simba akitokea Lipuli kwenda vizuri, lakini majeraha yalimuweka nje kwa muda mrefu na kufanya apoteze nafasi.