Uko hapa: NyumbaniMichezo2019 06 15Article 471648

Sports News of Saturday, 15 June 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz

Sunday Manara: Haji Manara asiwasumbue kalelewa na Yanga

Dar es Salaam. Haji Manara, msemaji wa klabu ya Simba ni kati ya binadamu wanaotikisa zaidi mitandao ya kijamii nchini kutokana na kauli zake za majigambo kuhusu mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati Haji akiwa kinara mitandaoni leo Jumamosi Juni 15, 2019 baba yake mzazi, Sunday Manara amezungumza jambo ambalo huenda likamtesa mwanaye, si ajabu watu kuanza kumtania.

Akizungumza katika harambee ya kuichangia Yanga iliyopewa jina la ‘Kubwa kuliko’ , Sunday ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo  kutosumbuka na kile alichokiita kelele za Haji kwa maelezo kuwa mwanaye huyo amelelewa na Yanga.

Sunday maarufu Kompyuta amesema kila wakati amekuwa anapokea malalamiko kutoka kwa mashabiki wa Yanga kuhusu mwanaye kuisema vibaya timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam.

Amewataka mashabiki wa timu hiyo kutambua kuwa Yanga ndio imemlea Haji.

Akifafanua zaidi kauli yake hiyo, Sunday amesema Haji alizaliwa wakati yeye akiicheza Yanga.

Pia Soma


Join our Newsletter