Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558253

Soccer News of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TANZIA: Rais wa zaman TFF afariki

Aliekuwa Mwenyekiti wa FAT (sasa TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga Aliekuwa Mwenyekiti wa FAT (sasa TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga

Aliekuwa mwenyekiti wa Chama Cha Soka Tanzania FAT, Alhaji Muhidin Ndolanga amefariki dunia katika Hopitali ya TMJ, Mikocheni Jijini Dares Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika kipindi cha Uhai wake Ndolanga amewahi kushika wadhifa wa juu kabisa wa Chama cha Soka nchini FAT( sasa hivi ni TFF) na amepewa Urais wa heshima wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini.

Ndolanga atazikwa Jumapili Septemba 19, Kibaha Mkoani Pwani.