Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584539

Habari za michezo of Monday, 10 January 2022

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

TETESI: Cristiano Ronaldo aanza mchakato wa kuhama Man United

TETESI: Cristiano Ronaldo aanza mchakato wa kuhama Man United TETESI: Cristiano Ronaldo aanza mchakato wa kuhama Man United

Wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes ametua nchini Uingereza kufanya mkutano na nyota huyo wa Man United kufuatia penyenye kuwa mteja wake anataka kuhama klabu hiyo.

Cristiano Ronaldo amefungia Man United magoli 14 katika mashindano yote muhula huu kuwazidi wachezaji wengine kwenye timu hiyo, Lakini kuna tetesi kuwa huenda ataagana na Mashetani Wekundu kwa mara ya pili iwapo timu hiyo itafuzu kushiriki Ligi ya Uropa muhula ujao.

Wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes kwa sasa yuko Uingereza kufanya mkutano naye kujadili mustakabali wake ujao katika klabu hiyo

Ronaldo amefungia Man United magoli 14 katika mashindano yote muhula huu kuwaliko wachezaji wengine kwenye timu hiyo.

Lakini kuna penyenye kuwa huenda ataagana na Mashetani Wekundu kwa mara ya pili iwapo timu hiyo itafuzu kushiriki Ligi ya Uropa muhula ujao.

Kwa mujibu wa ripoti ya Express UK na The Sun, huenda Ronaldo atalazimika kuondoka United miezi michache baada ya kurejea kutokana na masaibu yanayozonga klabu hiyo kwa sasa.

Inaaminika kuwa Ronaldo hafurahishwi na mbinu ya Rangnick kufunza timu hiyo.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or ameanza kujutia hatua yake ya kurejea katika klabu hiyo aliyojiunga nayo akiwa na umri wa miaka 18.

Rangnick amekuwa akikumbana na masaibu tangu kutua Old Trafford akipigana na mrupuko wa maambukizi ya virusi vya Corona ambao ulishuhudia uwanaja wa mazieiz wa klabu hiyo Carrington ukifungwa kwa zaidi ya wiki moja.

Mjerumani huyon alikabidhiwa mikoba ya Ole Solskjaer ambaye alipigwa kalamu sabbu ya kusajili matokeo duni ugani Old Trafford ambapo Red Devils walipoteza michezo muhimu.

Cristiano Ronaldo sasa hafurahishwi na mbinu ambazo kocha huyo mpya ameletea Manchester United.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa Cristiano Ronaldo anawazia kuondoka Manchester United huku Barcelona ikisemkana kuwasiliana na nguli huyo wa zamani wa Real Madrid.