Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 20Article 558616

Soccer News of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TETESI: Kaze anukia Jangwani

Cedrick Kaze Cedrick Kaze

Imeelezwa kuwa Cedrick Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga atarejea ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi.

Kaze alikuwa ndani ya Yanga msimu uliokwisha wa 2020/21 ambapo hakuweza kukamilisha mzunguko wa pili baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua kumfungashia virago.

Kwa mujibu wa Yanga walieleza kuwa Kaze alishindwa kuwapa kile ambacho walikuwa wanafikiria jambo ambalo liliwafanya waweze kufikia makubaliano ya kuachana naye.

Mechi yake ya mwisho alishuhudia vijana wake wakigawana pointi mojamoja dhidi ya Polisi Tanzania na bao la Yanga lilifungwa na mchezaji Fiston Abdulazak ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho.

Taarifa zimeeleza kuwa Kaze anarejea Yanga akiwa ni kocha msaidizi huku Kocha Mkuu akibaki kuwa Nasreddine Nabi.

Alipotafutwa Kaze ili aweze kuzungumzia jambo hilo hakuwa tayari kufunguka ishu ilivyo.