Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 14Article 557287

Habari za michezo of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

TFF kushirikiana na wadau kuboresha viwanja vya michezo

TFF kushirikiana na wadau kuboresha viwanja vya michezo TFF kushirikiana na wadau kuboresha viwanja vya michezo

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wilfred Kidau amesema shirikisho hilo litaendelea kushirikiana na wadau na wamiliki wa viwanja vya michezo nchini ambavyo viko chini ya viwango ili kuviboresha

Kidau alitoa kauli hiyo wilayani Karagwe katika Fainali za Bashungwa Karagwe cup wakati akijibu ombi la aliyekuwa mgeni Rasmi katika mashindano hayo Waziri wa Maji Jumaa Aweso aliyetaka kujua ni kwa jinsi gani TFF wataboresha uwanja wa wilaya ya Karagwe ambao unatumika kwa mashindano mbalimbali ya Mpira wa Miguu.

Akishuhudia Fainali hizo Aweso alisema Mashindano ya Bashungwa Karagwe Cup mashindano hayo yameibua vipaji vingi Baada ya vijana mbalimbali kusajiliwa katika timu Tofauti hapa nchini na kuipeleka timu ya Nyaishozi kufanikiwa kufuzu Hadi Daraja la Pili katika Ligi ya hapa nchini.

Alisema kama uwanja huo utaboreshwa vijana watacheza kwa kujiamini na Serikali itapata mapato kwani kwa Sasa Serikali haiingizi chochote kutoka na uwanja huo kutokidhi viwango vya mashindano ya kimataifa na Halmashauri ya Karagwe inapoteza mapato kwa kiwanja icho kutokuwa Bora.

Uwepo wa Mtendaji mkuu wa TFF Ni kuhainisha vipaji ambavyo vinapatikana katika mashindano hayo ambapo alisema kuwa kupitia vikao vilivyofanywa na serikali Ni kuwa kunampango wa kurejesha mashindano ya Taifa Cup yanayowashirikisha vijana hivyo vijana wajiandae kupigania vipaji vyao na Hakuna kipaji kitakachopotea hata Kama kijana anatokea pembezoni mwa nchi.

Mratibu wa mashindano hayo ambaye Ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe na waziri wa Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa alisema Mashindano hayo yameanza tangu mwaka 2017 na yameibua vipaji vingi Sana japo changamoto kubwa iliyopo Ni uwanja wa kuendesha mashindano hayo.

Kwa mwaka 2021 mashindano hayo yalihusisha timu 23 kutoka kata 23 ambapo timu zilipata jezi ,mipira na uwezesho wa kufika Uwanjani huku timu ya Nyabionza na Bugene ndizo zilibahatika kufika Hadi Fainali ,na timu ya Kihanga na Kanoni zikibahatika kufuzu kutafuta mshindi wa tatu.

Bugene ndio mabigwa ambao wametwaa kombe kwa mwaka 2021 na walipata kombe na kitita Cha Shilingi Milioni 2.5 , Nyabionza mshindi wa pili kitita Cha Shilingi Milioni 1.5, Kihanga Mshindi wa tatu shilingi laki 7.5 na Kanoni mshindi wa nne zawadi ya shilingi laki tano.

Hata hivyo Mgeni Rasmi Aweso alikabidhi zawadi za washindi ,timu yenye nidham Bora,waamuzi,mfungaji Bora,Golikipa Bora,mwalimu Bora wa timu,huku wadau mbalimbali wakionyesha kufurahishwa na mashindano hayo na kuunga mkono juhudi za Mbunge wa Jimbo Hilo mkono kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo.