Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 25Article 559624

Habari za michezo of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: ippmedia.com

TFF na Wizara ya Afya kutoa chanjo uwanjani

TFF na Wizara ya Afya kutoa chanjo uwanjani TFF na Wizara ya Afya kutoa chanjo uwanjani

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeingia makubaliano na Wizara ya Afya kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika vita dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa uviko 19.

TFF kwa kushurikiana na wizara hiyo imeweka mahema kwa ajili ya upatikanaji wa huduma ya chanjo nje na ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Lakini pia TFF imetoa tiketi 100 na zawadi kama motisha kwa idadi hiyo ya mashabiki watakaokuwa wa kwanza wakupata chanjo ya COVID 19.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, alisema wameamua kuunga juhudi za serikali za ili kupambana na ugonjwa huo ambao umesababisha mashabiki kutoingia uwanjani.

Kidao alisema wameanza kampeni hiyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa leo kwa kuwakutanisha Simba na Yanga na baadaye wataendelea kuhamasisha katika michezo mingine inayofuata ikiwamo ya kimataifa.

Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya ambaye pia ni Mratibu wa Afya Dar es Salaam, Agnes Mgaya, alisema wanaishukuru TFF kwa jitihada walizozionyesha katika kupambana na ugonjwa huu ambao umekuwa tishio.