Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 18Article 558157

Soccer News of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

TP Mazembe kutua leo mchana

Kikosi cha TP Mazembe safarini kuja Dar es Salaam Kikosi cha TP Mazembe safarini kuja Dar es Salaam

Msafara wa watu 35, wa Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka nchini Congo wameanza safari Kuja Tanzania katika maadhimisho ya kilele cha Simba Day.

Katika msafara huo umejumuisha wachezaji 23, wameanza safari kutokea nchini Congo hadi Addis Ababa, Ethiopia, kisha kesho saa 7 mchana, siku ya Jumamosi watatua jijiji Dar es Salaam.

TP Mazembe watacheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na Simba SC siku ya Jumapili Septemba 19 katika kilele cha Tamasha la Simba Day.

TP Mazembe ndio Mabingwa wa Ligi Kuu DR Congo, Ubingwa ambao walipokwa klabu ya AS vita.