Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 559021

Habari za michezo of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

TP Mazembe wafunguka Simba kufika mbali "Ligi ya Mabingwa"

NYOTA wa TP Mazembe, Rainford Kalaba NYOTA wa TP Mazembe, Rainford Kalaba

NYOTA wa TP Mazembe, Rainford Kalaba, ameitabiria makubwa Simba kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Kauli ya Kalaba imekuja muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki ambao TP Mazembe waliifunga Simba bao 1-0, juzi Jumapili kwenye Kilele cha Simba Day, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kalaba alisema: “Simba wamecheza vizuri na wana timu nzuri pia, naona wakifanya tena vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tatizo lao ni kushindwa kutumia vema nafasi walizotengeneza, hiyo ndiyo kasoro ambayo mimi binafsi nimeiona.”