Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 585025

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

TPLB yafanya mabadiliko michezo ya Ligi Kuu

Kagera vs Simba watamenyana Januari 26 Kagera vs Simba watamenyana Januari 26

Mchezo namba 69 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi Simba SC dhidi ya Kagera Sugar umepangiwa tarehe mpya baada ya kuahirishwa.

Mchezo huo uliokua umepangwa kuchezwa Desemba 18 mwaka 2021, uliahirishwa kufuatia changamoto za kiafya iliyowakumba baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakiwa mjini Bukoba.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara TPLB imetoa marekebisho madogo ya ratiba leo Jumanne (Januari 11), ambayo yanaonyesha mchezo huo utachezwa Januari 26, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

Mabadiliko hayo pia yamehusisha michezo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya Makundi ambapo Simba SC itashiriki kuanzia mwezi Februari.

Tazama hapa chini Taarifa ya Bodi ya Ligi inayojieleza kwa kirefu;