Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 14Article 542620

Habari za michezo of Monday, 14 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Taifa Stars yaanza kunoga

Taifa Stars yaanza kunoga Taifa Stars yaanza kunoga

Ulikuwa ni mchezo wa kirafiki ulio kwenye Kalenda ya FIFA, ukipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Nahodha John Bocco aliifungia Stars bao la kwanza dakika ya 68 baada ya kupata pasi tamu kutoka kwa Kibu ambaye alikuwa amemnyang'anya beki mmoja wa Malawi mpira karibu na eneo la hatari, kabla ya kuvuta hatua tatu na kutoa pasi murua kwa mfungaji.

Mchezaji huyo aliyeingia badala ya Salum Aboubakar 'Sure Boy', aliangushwa nje kidogo ya eneo la hatari dakika sita baadaye na kuwa faulo ambayo ilipigwa na Israel Patrick Mwenda na kuujaza wavuni na kumuacha kipa Brighton Muntali akishangaa.

Mpira ulianza kwa kasi na kwenye sekunde ya 30 tu, nahodha Bocco alimiminiwa krosi kutoka kwa Shomari Kapombe, lakini akapiga kichwa mpira ukatoka juu ya lango la Malawi ambayo katika viwango vya ubora vinavyotolewa na Fifa ipo nafasi ya 115 kwa mwezi uliopita huku Tanzania ikiwa nafasi ya 137.

Yusuph Mhilu naye alikosa bao la wazi dakika ya tano, akipiga mpira nje ya lango baada ya kubaki na kipa wa Malawi, Muntali. Taifa Stars iliendelea kutawala kabumbu, huku Malawi ikionekana kusoma mchezo na ilianza shambulio la kwanza dakika ya 22.

Alikuwa ni mchezaji anyecheza soka la kulipwa nchini Urusi kwenye klabu ya Sheriff Tiraspol, Peter Banda, alipoupata mpira uliookolewa na mabeki wa Stars akiwa nje kidogo ya eneo la hatari, akapiga shuti la kiufundi, lakini ukitoka juu kidogo ya lango. Mchezaji huyo anacheza timu hiyo kwa mkopo akitokea Big Bullets FC ya nchini Malawi.Aishi Manula aliiokoa Stars kufungwa dakika ya 38 alipopangua shuti kali la mbali na kuwa kona tasa.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko, Stars ikiwatoa Erasto Nyoni, Sure Boy, Shomari Kapombe, Yusuph Mhilu, Nickson Kibabage na Mudathir Yahaya na nafasi zao kuchukuliwa na Kennedy Juma, Kibu, Ayoub Lyanga, Mwenda, Mzamiru Yassin na Abdul Selemani, mabadiliko ambayo yaliisaidia sana Stars chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

Habari

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni