Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560131

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Takwimu zaibeba Simba mechi dhidi ya Biashara

Takwimu za mechi baina ya Biashara na Simba SC Takwimu za mechi baina ya Biashara na Simba SC

Pazia la Ligi kuu limefunguliwa Septemba 27 kwa kushuhudia mechi tatu katika viwanja tofauti ikiwemo Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga, Uwana wa Ilulu Lindi na Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wapo kule Musoma mkoani Mara kuwakabili Biashara United Mkoani Mara.

Wakati Simba wakijiandaa kukabiliana na Wanajeshi hao wa Mpakani majira ya saa 10:00 leo Jioni, rekodi zinaonesha Biashara United hawafanyi vizuri wanapokutana na Simba.

Tangu 2019, Biashara United hajawahi kupata Ushindi mbele ya Simba SC. Katika michezo 6 waliyokutana, Wamefungwa michezo 5 na kupata sare 1.

Lakini pia katika mechi hizo 6 walizokutana, Simba wamefungwa Jumla ya Mabao 13 huku wao wakifunga Mabao 2 tu

Huenda muda ukatupa majibu sahihi iwapo Biashara itafuta uteja kwa Simba hii leo ama Mnyama ataendeleza rekodi zake kwa Biashara.