Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 552031

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Tambwe arejea soka la Bongo

Aliekua Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe Aliekua Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe

DTB FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, imethibitisha nia yao ya kumrudisha nchini straika maarufu Mrundi, Amissi Tambwe.

Tambwe aliyewahi kucheza katika klabu za Simba na Yanga anasifika kwa utupiaji nyavuni na Katibu Mkuu wa DTB, Muhibu Kanu amesema; “Ni kweli tuko kwenye mazungumzo, tukikubaliana atakuja.”

Habari za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu na mchezaji huyo alilidokeza Mwanaspoti kwamba Tambwe anarejea nchini wakati wowote kuanzia jana baada ya kumalizana kila kitu na mmoja wa vigogo wa timu hiyo.

“Tambwe anarejea nchini kuanzia wiki hii, ameshaelewana kila kitu na bosi wa timu hiyo na anakuja kusaini mkataba, ameamua kuja huku kwa sababu ameona timu hiyo inajipanga kupanda Ligi Kuu,” kimesema chanzo hicho.

Wakati huo huo, inaelezwa vigogo wa klabu hiyo wapo kwenye mipango ya kumrejesha nchini Tafadzwa Kutinyu, raia wa Zimbabwe aliyewahi kucheza Singida United na Azam FC.