Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 22Article 552913

Soccer News of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Tambwe kajipanga Championship, Kutua Tanzania

Mshamuliaji wa DTB, Amissi Tambwe Mshamuliaji wa DTB, Amissi Tambwe

Huku kila timu ikijiwinda kutengeneza Kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/2022, Timu inayozungumzwa sana midomoni mwa watu kwa sasa ya DTB ,inamshusha Straika wake hatari Amissi Tambwe siku ya jumapili Agosti 22.

DTB moja ya timu zilizowashangaza wadau wengi wa kandanda kutokana na aina ya wachezaji ambao inawasajili kwa ajili ya kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Katika mahojiano yake na mwandishi wa habari, Tambwe ambaye ametbibitisha kurejea ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine akiwa na timu ya daraja la chini akiamini kwa ushirikiano na wenzake watafikia malengo ya kupanda daraja kwa timu hiyo ili kucheza Ligi kuu.

"Nakuja Tanzania Jumapili, ni kweli nitakuwa mchezaji wa DTB, mpira ndio kazi yangu timu yoyote ikinihitaji tukakubaliana nacheza tu wala sina ubaguzi katika hilo," amesema Tambwe.

Tambwe amesema analijua vyema aina ya soka la Tanzania kwa ujumla linahitaji ushindani mkubwa na nguvu zaidi ili kuweza kuonyesha uwezo uwanjani.

"Ligi ya Tanzania imekuwa maarufu sana na inaonekana kutokana na kutangazwa zaidi tofauti na huko nyuma, hivyo inawafanya watu wengi kuifuatilia zaidi," amesisitiza.

Amesema yeye kama mwanakandanda anafarijika kurejea sehemu ambayo anajua na kutambua namna gani ya kucheza hivyo hiyo ni fahari kubwa kwake katika majukumu yake kikazi.

"Mimi namshukuru sana Mungu Tanzania najulikana sana, na watu wananitambua na wanajua kazi yangu, sina ugeni wowote na pia inawafanya watu waifuatilie hiyo timu zaidi,"

Wakati huo huo Tambwe amesema, usajili wa Yanga ni mzuri lakini cha msingi akisisitiza ligi itakapoanza ndipo watajua na kuona ubora wa waliowasajili.

"Kusajili ni kitu kingine na kufanya vizuri ni jambo lingine, ligi ikishaanza ukiwatazama wanavyocheza na matokeo wanayoyapata ndiyo yatakupa tafsiri ya usajili ulioufanya," amesema Tambwe.

Hamis Tambwe kwa nyakati tofauti amewahi kuvichezea vilabu vikongwe vya Tanzania Simba na Yanga na kupata navyo mafanikio makubwa.