Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 23Article 559306

Habari za michezo of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Tamko la Simba SC kuhusu takwimu za bodi ya ligi Kuu Tanzania bara

Tamko la Simba SC kuhusu takwimu za bodi ya ligi Kuu Tanzania bara Tamko la Simba SC kuhusu takwimu za bodi ya ligi Kuu Tanzania bara

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) leo imetangaza Club 20 za soka Tanzania ambazo zimeingiza Mashabiki wengi viwanjani (home ground) katika msimu wa 2020/2021.

1- Yanga SC Mashabiki 141,681

2- Simba SC Mashabiki 138,518

3- Dodoma Jiji FC Mashabiki 27,455

4- JKT Tanzania Mashabiki 25,062

5- Mwadui FC Mashabiki 22, 232

Hizi ni baadhi ya Club ila orodha iliyotangazwa inafikia Club 20.

Kwa upande wa mapato Bodi ya Ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) ikataja Club za soka zilizopata mapato mengi kupitia viingilio vya mlangoni kwa msimu mzima wa 2020/2021

1- Yanga SC Tsh millioni 986.8

2- Simba SC Tsh milioni 929.7

3- JKT Tanzania Tsh milioni 148.1

4- Dodoma jiji Tsh milioni 139.3

5- Ihefu FC Tsh milioni 138.6

Hizi ni baadhi ya Club ila orodha iliyotangazwa inafikia Club 20.

Kufuata takwimu hizo sasa Afisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga kafunguka kuhusiana na namna walivyoipokea taarifa hiyo.