Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 16Article 558001

Soccer News of Thursday, 16 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Tanzania yapanda viwango vya FIFA

Kikosi cha Taifa Stars Kikosi cha Taifa Stars

Tanzania imepanda kwa nafasi tatu katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Septemba.

Kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotangazwa leo Septemba 16, Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 135 hadi ya 132 na kuzipiku nchi za Togo, Lithuania na Comoro ambazo zilikuwa juu yake katika viwango vya ubora vya mwezi uliopita.

Nafasi hiyo imekuja kutokana na Tanzania kucheza mechi mbili na kutoa sare na DR Congo na ushindi dhidi ya Madagascar.