Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572494

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tanzania yapoteza kwa penati soka la ufukweni

Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni

Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) imepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mozambique katika mashindano ya COSAFA yanayoendelea nchini Afrika ya Kusini.

Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya magoli 4-4, umeamuliwa kwa njia ya mikwaju ya penati.

Tanzania imepoteza kwa penati 4-3 na mechi yao itayofuata watacheza dhidi ya Comoro saa 10:30 jioni ya leo.