Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572629

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tanzania yatinga nusu Fainali Soka la ufukweni

Tanzania yatinga nusu fainali Soka la ufukweni Tanzania yatinga nusu fainali Soka la ufukweni

Tanzania imefanikiwa kutinga nusu Fainali ya michuano ya Soka la Ufukweni ya COSAFA baada ya kufanya vizuri katika mechi zake za leo Jijini Durban, Afrika Kusini.

Mechi ya kwanza Tanzania ilishinda 2-1 dhidi ya Comoro kabla ya kufungwa kwa penalti 4-3 na Msumbiji kufuatia sare ya 4-4 ufukwe wa South Beach Arena.

Sasa Tanzania itamenyana na Angola katika mechi ya nusu Fainali Novemba 19, hapo hapo South Beach Arena, wakati Msumbiji itamenyana na wenyeji, Afrika Kusini katika nusu Fainali nyingine.