Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 04Article 561262

Kriketi of Monday, 4 October 2021

Chanzo: Mwanaspoti

Tanzania yazidi kung'ara michuano ya cricket

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Cricket Timu ya Taifa ya Tanzania ya Cricket

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Cricket chini ya umri wa maiaka 19 wameshinda mchezo wao wa tatu dhidi ya Nigeria katika michuano ya kusaka tiketi kushriki kombe la dunia kwa bara la Afrika nchini Kenya.

Akizungumza na Mwanaspoti Afisa Habari wa Chama cha Cricket Tanzania (TCA), Atiff Salimu anasema Tanzania imebakiza mechi moja dhidi ya Uganda utakaopigwa Oktoba 6.

“Timu yetu imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Uganda Oktoba 6 na kama tutapata ushindi tutakuwa tumefanikiwa kufuzu kombe la dunia la cricket kuwakilisha Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 19.

Huu ni mchezo wa tatu Tanzania wanacheza katika michuano hiyo ambapo mchezo wa kwanza walicheza dhidi ya mwenyeji Rwanda na Tanzania kushinda wa wickets 4 huku Gokul Das akiibuka mchezaji bora wa mchezo.

Mechi ya pili walicheza dhidi ya Namibia iliyokuwa moja ya timu tushio kwao na wakishinda kwa mikimbio 48 huku Laksh Barkani akitwa mchezaji bora wa mecho na mechi ya leo dhidi ya Nigeria wameshinda kwa wickets 9 na Yalinde Nkanya kuibuka mchezaji bora wa mechi.