Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586000

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tanzanite Queens Kazi inaendelea Zanzibar

Tanzanite Queens Kazi inaendelea Zanzibar Tanzanite Queens Kazi inaendelea Zanzibar

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake wa U20, Tanzanite Queens, imeweka kambi visiwani Zanzibar ikiwa ni maandalizi ya kuwavaa Ethiopia Januari 23 kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Kikosi hicho kilianza mazoezi yake kwenye Uwanja wa Amaan juzi jioni, kikiwa chini ya kocha Bakari Shime, kisha jana wakafanya tena mazoezi kwenye Uwanja wa Mao B.

Shime alisema wamekwenda kuweka kambi visiwani humo kwa sababu mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Amaan, kisha baada ya mchezo watasafiri kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano, mchezo ambao mshindi wa jumla atakwenda kwenye hatua ya tano na itabaki hatua moja kabla ya kupata tiketi.

“Mechi yetu itachezwa hapa Zanzibar, ndiyo maana tumekuja mapema ili vijana hawa wafanye maandalizi yao na kuzoea mazingira, muda wa zaidi ya siku 10, unatosha kabisa kwa maandalizi,” alisema.